HIVI NDIVYO VIGEZO VINAVYOWEZA KUSABABISHA MWANAUME KUKIMBIWA NA WANAWAKE?......KIDUME KUWA MAKINI NA VIGEZO HIVI | MAHUSIANO BLOG

HIVI NDIVYO VIGEZO VINAVYOWEZA KUSABABISHA MWANAUME KUKIMBIWA NA WANAWAKE?......KIDUME KUWA MAKINI NA VIGEZO HIVI


1. Wakikosa attention yako. Wasichana hupenda pale wanapofahamu kuwa unawasikiliza na unafahamu nini wao wanahitaji. Kama kutakosekana mawasiliano mazuri na atagundua hilo atauona uhusiano huo haumtimilizii haja zake. Hata kama kila kitu kinaenda sawa. Msikilize anapoongea. Kama akiona hapati penzi analolihitaji atatafuta mwingine ambaye yupo tayari kumtimizia.
2. Kumuheshimu. Msichana huwa anajitoa sana awapo katika mahusiano hivyo anategemea mvulana uheshimu hata kwa chochote kidogo anachokufanyia. Mfanye agundue kuwa umeheshimu kile ambacho amekufanyia.


3. Usaliti. Unaposaliti inamaanisha kuna kitu hakipo sawa katika mahusiano yako hata kama una uwezo wa kushughulikia lakini wewe unaona njia sahihi ni kutoka nje kuwa na mahusiano na msichana mwingine ukidhani ndio unarekebisha. Pale msichana wako akikukamata unamsaliti fahamu hawezi kuvumilia naye atakuacha.


4. Ukosefu wa hisia za kimapenzi. Msichana hupenda kuona kuwa wanapendwa wanathaminwa na wapenzi wao wanawajali sasa wakiona kuwa hakuna conection ya hisia za kimapenzi kutoka kwa mvulana wake huona kuwa hakuna mapenzi ya kweli katika uhusiano aliopo


5. Hawapendi kusikia kuhusu mapenzi mara kwa mara wasichana hupenda kutumia muda mrefu na wapenzi wao bila kusikia neno la kuwataka wafanye mapenzi kama ukiwa nao na ukawataka kimapenzi mara kwa mara watakuwa wanakuavoid hata utakapokuwa ukiwagusa.


6. Unapomcontrol sana
msichana humpenda mvulana atakayemlinda na kujiona yupo sehemu salama sio kumdhibiti kufanya mambo yake mengine anapenda uhuru.
-dira la mahusiano

0 Response to "HIVI NDIVYO VIGEZO VINAVYOWEZA KUSABABISHA MWANAUME KUKIMBIWA NA WANAWAKE?......KIDUME KUWA MAKINI NA VIGEZO HIVI"

Post a Comment