MWANAUME FANYA HAYA KUEPUKA KUFIKA KILELENI MAPEMA | MAHUSIANO BLOG

MWANAUME FANYA HAYA KUEPUKA KUFIKA KILELENI MAPEMALeo katika uwanja wa mahaba tutaangazia tatizo la mwanaume kuwahi kufika kileleni, sababu ya tatizo hili huweza kuwa ya kibaiolojia nakiakili. Kama wewe pia ni moja wao na unapenda kujua jinsi ya zuia hali hii, basi huna budi kuzingatia haya.

Kufanya mazoezi, mwili wenye afya nzuri daima hufanya kazi vizuri, kwa hiyo kitu rahisi cha kufanya ni kujenga tabia ya kufanya mazoezi ambayo husaidia kukujengea afya njema na kukupa mzunguko mzuri wa damu. Kama una mwili wenye afya basi inaweza kukusaidia kwa namna ya kifikra ambazo huchangia kwenye suala zima la kuwahi kufika kileleni. Hii hutokana na kuongeza kujiamini na kujihusudu.

Pumua vizuri na kikamilifu, kiungo chochote cha mwili huhitaji nguvu kamili ili kufanya kazi na ndivyo ilivyo kwa habari ya viungo vya uzazi! Unapopumua vizuri na kwa ukamilifu, kiungo hiki hupata nguvu za ziada. Jaribu kupumua kwa ufasaha ili mwili uweze kupata hisia kabla ya kuanza kufanya msuguano.

Mshirikishe mwenzako kikamilifu, kuridhika kimapenzi ni tukio ambalo wote wawili mnaridhika kikamilifu. Ili kujifunza kujizuia kufika kileleni haraka, ni vizuri kuwasiliana na mwenzi wako wa kimapenzi. Anaweza akakusaidia kushinda tatizo hili la kiaibu, kila unapohisi unataka kukojoa mapema, sema ‘ngoja’ na usitishe kwanza shughuli zote kwa muda kidogo.

Maandalizi kifikra, pia kabla ya kwenda kuanza tendo kwa mfano upo ofisini na unajua jioni unakwenda kufanya mapenzi basi jitahidi usiwaze hayo mambo chukulia kama ni kitu cha kawaida.

Hii ni kwa sababu kuongeza ari ya kuwaza tendo la ndoa pia inaongeza msisimko kiasi kwamba ukimgusa mpenzi wako tayari umekwishaachia hata kabla ya kuingiza.

Angalia movie, kuangalia ‘style’ zenye kuchochea kufika kileleni haraka hii ni ngumu kujizuia kukojoa hasa kwa bao la kwanza maana panakuwepo na msuguano wa hali ya juu kiasi kwamba ukigusa tu tayari kwa hiyo ni vizuri ‘style’ kama hizi zikafuata baada ya bao la kwanza ili uweze ku-enjoy vizuri zaidi.

0 Response to "MWANAUME FANYA HAYA KUEPUKA KUFIKA KILELENI MAPEMA"

Post a Comment