NJIA 5 ZA KUMFANYA MWANAMKE AKUFUKUZIE BAADA YA KUMUONESHA HISIA | MAHUSIANO BLOG

NJIA 5 ZA KUMFANYA MWANAMKE AKUFUKUZIE BAADA YA KUMUONESHA HISIA

Najua huwa tunatumia muda mwingi sana vijiweni tukiongelea, sehemu gani nzuri ya kukutana na wanawake, jinsi ya kuwatongoza na kuanzisha maongezi, nini cha kuongea na kufanya ili akuelewe na mrembo awe wako, Lakini hayo yote ambayo huwa tunayaongelea huwa ni kama theluji kwenye mlima Kilimanjaro, ila volkano yenyewe huwa ni jinsi ya kuwafanya wanawake waanze kukuhangaikia na kukufuatilia, na hizi hapa ni njia tano za kuwa wapekee na kuwafanya watoto wenyewe wa kike wawe wanakuhangaikia.
Naomba nitilie mkazo jambo moja, njia hizi hakikisha hauzichukulii juu juu, zielewe na zitunze vizuri kwenye akili yako, maana unahitaji kila kitu uwe umeshakielewa kwa yote tuliozungumzia hapa kiumeni kuhusu wanawake.
Namba 1. Tengeneza mvuto unaovutia kwake mara ya kwanza unaongea nae.
Sifa ya mwanaume wa kweli huwa ni kujiamini, na mwanamke sikuzote anavutika na mwanaume wa kweli, onyesha kujiamini na kuwa mkufunzi wa mchezo wa Kutongoza toka moyoni bila hata kufikiria utaongea nini au kujishitukia, utaona mwanamke mwenyewe hata kama angekuwa amekutegea mgongo atageuka na kuanza kukusikiliza kwa mvuto, mkibadilishana namba kesho mwenyewe ndo atapiga simu na kuanza kujitambulisha, “Halo, mie ndo yule dada tuliobadilishana namba”, mwenyewe anaanza kujinogesha, kukufatilia na kukuwinda.
Namba 2. Muonyeshe changamoto.
Mwanamke akihisi wakati unamtongoza kuwa umeshakufa kwake ukaoza, huna mwingine yeye ndio yeye, unamuhitaji kupitiliza kwa hiyo utafanya chochote, moja kwa moja anakuweka kwenye kundi la FALA, (Samahani kwa kutumia kiswahili kibaya, ila ndo hivyo), mwanamke sikuzote huwa havutiki na mwanaume Fala, mwanaume ambaye mapenzi yanamuendesha.
Namba 3. Muulize maswali ya namna flani.
Mwanamke akishakusoma na kukuona wewe ni mwanaume wa aina flani, kuna uhakika mkubwa ataendelea kukufikiria kuwa wewe ni mwanaume wa aina hiyo, kwa hivyo ukianza kuonyesha tokea mwanzo we ni mwanaume yule anaye lilia mapenzi, basi ataanza kukuona fala tokea mwanzo, mwanaume ambae utamfuata fuata hata pale ambapo hautakiwi, na unajua wanawake wanahisia gani na wanaume wa aina hii. Kwahiyo ukianza na maswali ya kuonyesha tabia ya kifala, patishia huyo mwanamke ataanza kukufikiria kuwa utakuwa na tabia hizo hizo kwa kipindi chote cha maisha yako, na huo ndo utakuwa mwisho wako.
Namba 4. Usimfuatilie sana.
Usipoonana na mtu sana mara kwa mara hukufanya uanze kumkumbuka, na hii kanuni ukiitumia vizuri kwa mwanamke utamfanya aanze kukuulizia kwa rafiki zako, iwapo ungeitumia hata kwa naniii hata hizo meseji ambazo hakujibu angekuwa anazijibu. Iwapo ukiwa unapendelea kumuona ona huyo mwanamke, au husubiri na kumpa muda mwanamke kumpigia simu mara baada ya yeye kukupigia, utafanya siku zote uwe kwenye uhusiano wa upande mmoja.
Namba 5. Muonyeshe umempa akili yako na umakini kwa hali flani. Wanawake wanapenda sana wakiwa wanaongea na mwanaume, na mwanaume huyo akawa anawapa umakini wa kuwasikiliza. Tofauti na hapo wanawake huwa wanaishiwa mvuto na mwanaume ambae anawapa umakini kiasi cha kupitiliza, umakini huu sio wa kusikiliza bali ule wa kuonyesha wewe ndo unaejua kupenda kwa kumpa sifa nyingi katika hali ambayo hazihitajiki

0 Response to "NJIA 5 ZA KUMFANYA MWANAMKE AKUFUKUZIE BAADA YA KUMUONESHA HISIA"

Post a Comment