WASICHANA WA SEKONDARI NI HATARI SANA KWA SASA TUWE MAKINI..TAZAMA ANACHOKIFANYA HUYU APA | MAHUSIANO BLOG

WASICHANA WA SEKONDARI NI HATARI SANA KWA SASA TUWE MAKINI..TAZAMA ANACHOKIFANYA HUYU APA

Habari wanajamvi.
Ngoja nami niwe mtoto kidogo kwa kusimulia na kutoka kasiri ka mambo ya kitoto.
Wiki iliyopita nilikuwa natoka zangu Mbeya kuelekea Dar es salaam kwa basi moja hivi.
Jirani yangu kwenye siti alikuwa amekaa "katoto" flani ka kike kama ka miaka 17-19.
Yule mtoto alikuwa mstaarabu sana. Akaniamkia kisha akatulia. Gari lilipoondoka akaanza kunisemesha. Akaniuliza ninapokoka, niendako, origin yangu na maswali kibao ya kizushi. Akajitambulisha kuwa yeye ni mwanafunzi wa kidato cha nne alikuwa anaumwa akarudi nyumbani anaelekea shuleni(akataja jina la shule).
Njiani nikawa nikinunua maji namnunulia, nikinunua kitu chochote naye namnunulia. Safari ikaendelea.
Tulipofika Morogoro akaniomba nimwazime simu yangu afanye mawasiliano kwani yake haina credit. Bila hiyana nikampatia akaitumia akanirejeshea.
Kwa kweli nilimchukulia kama mdogo wangu tu hadi tunafika.
Kituko kikaanza usiku kama saa 6:30 usiku hivi, nikiwa nimelala ikaingia message kwenye simu yangu "mimi yule dada tuliyesafiri wote leo, umefika salama nyumbani? Usiku mwema".
Kumbe katoto ka watu kalichukua namba yangu bila mimi kujua. Basi mtoto akatuma tena asubuhi kama saa 12:00 "vipi umeoa? Unaonekana mstaarabu, nimemiss sana jinsi ulivyo mpole, asubuhi njema".
Sikujibu chochote. Mchana akatuma message tena, jioni tena nami bila kujibu. Usiku wa siku ya pili kama saa tano usiku akapiga tena simu na kunitamkia anapenda tukutane aniambie jinsi gani alivyonipenda kimapenzi. Kisha akakata simu nami sikupiga.
Jioni nikamtumia message nikimpa ushauri na kumnasihi kuwa ajitahidi katika masomo yake na aache kufikiria kuhusu mapenzi.
Akakoma kupiga na kutuma tena message ila nikawa nimejifunza kitu kwa zile message alizokuwa anatuma. Utadhani kaandikiwa jinsi zilivyojaa maneno ya kimahaba ya kukata na shoka. Na jinsi message zilivyo huwezi amini kama kaandika mtoto wa sekondari.
Kama hali ndo ilivyo kwa mabinti zetu wanaosoma basi kazi tunayo wazazi na hatutavuna kitu kwa mabinti zetu wa aina hii.
CREDIT:JAMII FORUM

0 Response to "WASICHANA WA SEKONDARI NI HATARI SANA KWA SASA TUWE MAKINI..TAZAMA ANACHOKIFANYA HUYU APA"

Post a Comment