KWA MNAOCHEPUKA NA MUME WA MTU==>>HUU NDIO UZURI NA UBAYA WA KUCHEPUKA NA MUME WA MTU | MAHUSIANO BLOG

KWA MNAOCHEPUKA NA MUME WA MTU==>>HUU NDIO UZURI NA UBAYA WA KUCHEPUKA NA MUME WA MTU

Tumekutana tena kwa mara nyingine ili tuweze kupeana mawili matatu yanayohusu uhusiano wa kimapenzi na maisha ndani ya ndoa.
Kabla sijaingia chumba cha habari na kuandika makala haya, nilifanya utafiti mdogo kwa kuwashirikisha marafiki, wanafunzi na watu wengine walio na uzoefu wa maisha ya kimapenzi na baadaye kubaini sababu kadhaa zinazowafanya wasichana kupenda waume za watu.
Mabadiliko ya mtindo wa maisha, umeyafanya mapenzi kugeuka na kuwa kama kitu badala ya sanaa. Ndiyo, zamani watu walipenda mtu kutokana na mazingira, mtu mtiifu, mchapakazi, muadilifu, muaminifu na hata mwenye hulka ya kupenda ndugu wa pande zote mbili. Ndiyo maana, ilikuwa rahisi kwa wazazi kuchagua mwenza wa mtoto wao kwa kuzingatia mambo haya.
Lakini kadiri muda unavyokwenda na maisha kubadili mwelekeo, hivi sasa mapenzi hayana tena sifa hizo, isipokuwa nini mtu atapata kutoka kwa mpenzi wake, awe wa kike au wa kiume.
Wakati wengi hivi sasa wanatazama watakachopata ili kurahisisha maisha, wasichana wengi siku hizi wanapenda kutoka na watu wenye umri mkubwa zaidi yao na tena walio tayari kwenye ndoa, yaani waume za watu.
Sababu ni nyingi kwao, lakini mojawapo ya kinachowavutia kwa waume za watu ni kile wenyewe wanachodai wanajali. Kwamba, wanajali zaidi kuliko vijana ambao huzingatia tamaa zao za miili tu.
“Ni ukweli usiopingika kwamba vijana wa siku hizi wengi wanapenda sana kulelewa, kama huna fedha za kumpa au zawadi anakuona huna thamani kwake, yaani tumeshakuwa nao sana hao vijana, ukiona mpaka mtu ameamua kugeukia waume za watu ujue ameshachoshwa,” anasema Rose, mkazi wa Magomeni, Dar.
Licha ya kuwajali, lakini pia wadada wanadai waume za watu wanajua kuhudumia. Kuna suala lingine la kujiamini pia. Eti waume za watu wanajiamini, kwani licha ya kuwa na wake zao, lakini hawaoni tabu kuwatambulisha nyumba ndogo zao kwa marafiki na hata ndugu, tofauti na vijana ambao kutokana na ‘ukicheche’ wao, huwa ngumu kwao kwani wanaamini wakiwa wazi wataumbuka.
Wasichana wengi pia wanakimbilia kwa waume za watu kwa madai wana mapenzi ya dhati na wanajali. Kwamba wanaume hawa wakimfuata msichana, humweleza ukweli kuwa wako katika ndoa, hivyo ni jukumu lao kukubali au kukataa na hata wakiahidi kitu, ni rahisi kutekeleza tofauti na vijana wengi walaghai.
Pia, kutokana na uzoefu wao wa maisha, wasichana wanaamini wanaume hawa huwa na ukomavu zaidi wa kiakili na mara nyingi huwashauri wapenzi mambo ya kimaendeleo, tofauti na vijana.
Lakini pamoja na faida ambazo wasichana wanadai kuzipata, kitendo cha kuwa na uhusiano na waume za watu ni hatari hasa wake zao wakibaini, pia ni kujivunjia heshima hivyo nawashauri waache kujiingiza kwenye mapenzi ya aina hiyo.

0 Response to "KWA MNAOCHEPUKA NA MUME WA MTU==>>HUU NDIO UZURI NA UBAYA WA KUCHEPUKA NA MUME WA MTU"

Post a Comment